Mechi kati ya Manchester united na Manchester city iliyotarajiwa kuchezwa leo jijini Beijing imeaihirishwa kutokana na hali mbaya ya uwanja.
Tovuti ya Manchester united kutoka England ilithibitisha kuwa mechi kati ya timu hizo haitachezwa kutokana na hali mbaya katika uwanja.
"Kutokana na hali mbaya ya uwanja, kikundi cha mashindano na timu shiriki zimekubaliana kuhairishwa kwa mechi." Kilisema chanzo
Hata hivyo Mourinho aliongeza kuwa matokeo ya kujiandaa na mechi za ligi hayana umuhimu kulinganisha na afya ya wachezaji wake.
"Dhumuni langu ni kurudi na wachezaji wakiwa salama nadhani matokeo ya mechi hizi si muhim kama kurudi nao England salama." Alisema Mourinho.

Comments
Post a Comment