Timu ya Yanga imeendelea kuboronga katika mechi za makundi baada ya kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama.
Katika mchezo huo Yanga ilianza kupata bao kupitia Mshambuliaji wake Donald Ngoma katika dakika ya pili ya mchezo hata hivyo Medeama ilisawazisha bao hilo kwenye dakika 17 baada ya Ofori kutumbukia nyavuni.
Yanga imeshindwa kutamba kwenye michezo miwili ya nyumbani baada ya kufunga na TP Mazembe na kutoa kwenye mchezo wa leo, hivyo wana kibarua kizito dhidi ya miamba hao ugenini.
TP Mazembe ndiyo inayo ongoza kundi hilo ikiwa na pointi 6, ikifuatiwa na MO Bejaia yenye ponti 4, Medeama yenye pointi 2 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 1.

Comments
Post a Comment