Mkhitaryan: Nitakua fundi Man united


Kiungo mpya wa Manchester united Henrik Mkhitaryan amesema kuwa  atazidi kuimarika katika timu ya Manchester united.

Mkhitaryan alicheza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan ambapo Manchester united iliibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2-0.

"Manchester united ni timu bora, pia kuna ushirikiano mzuri na wachezaji wenzangu nadhani siku hadi siku nitakuwa bora." Alisema Mkhitaryan

Mkhitaryan alijunga na Manchester united akitokea Borussia Dortmund ya Ujermani kwa mkataba wa miaka minne.

Comments