Mohamed Dewji ameweka wazi nia yake ya kuwekeza Simba akiitaka timu hiyo imuuzie hisa kwa asilimia 51.
Dewji maarufu kama MO anataka kuwekeza kiasi kisichopungu bilioni 20 za kitanzania ili Simba iweze kunyanyuka.
MO mbele ya waandishi wa habari alisema anaumia sana kuiona Simba ikipoteza uelekeo na kushindwa katika soka.
"Uwekezaji wa milion 500 ni mdogo sana, Nataka kununua asilimia 51 ya hisa nataka kuwekeza bilioni 20 ili tuzalishe na kupata faida."
"Kila siku nimekuwa nikisema kuwa Simba inahitaji mwekezaji na siyo mdhamini, nadhani timu ninayoipenda inakwenda kugomboka." Aliongeza Mo
Mohamed Dewji ndiye mmiliki wa kampuni ya Mohamed Enterprises Company Limited (METL) ambayo inasambaza bidhaa mbalimbali Tanzania ikiwemo unga na ngano.

Comments
Post a Comment