Mourinho aingia kazini Rasmi


Kocha wa Manchester united Jose Mourinho amewasili leo katika jiji la Machester kuanza kazi rasmi na timu hiyo.

Mourinho alionekana akiwasili majira ya asubuhi sana na moja kwa moja alielekea kunako ofisi za timu hiyo kuanza majukum yake.

Mourinho alituma picha za mnato pamoja na video zilizomwonesha akiwasili jijini hapo katika akaunti yake ya Instagram.

Kocha huyo anatarajiwa kufanya mahojiano na vyombo vya habari siku ya nne ikiwa ni sehemu ya kwanza ya kuanza kutekeleza majukumu yake.


Comments