Kocha wa Manchester united Jose Mourinho amesema kuwa atamsuka beki Eric Bailly aliyemnunua kutoka Villareal alingane na Rafael Varane wa Real Madrid.
Bailly alicheza chini ya kiwango katika mechi ya kirafiki dhidi ya Wigan katika dimba la DW, licha ya kupewa dakika 82 katika mchezo lakini hakuweza kuonesha cheche zake.
"Nitafanya kila jambo ili kuhakikisha Bailly anakuwa bora kama nilivyowahi kufanya kwa mabeki wengine wa kati kama Varane." Alisema Mourinho.
"Ni kijana mdogo ambaye alionesha kitu kwenye soka, nasi tukaamua kumnunua, ni mara yake kwanza kuvaa jezi ya Manchester united, hafaa kiingereza mara nyingi anaelewana na wachezaji wanaozungumza kifaransa pamoja kispaniola." Aliongeza Mourinho.
Mourinho alisema atampatia dakika nyingi za kucheza beki huyo ambaye alitua kwa dau la uhamisho wa Euro 30 Milioni kutoka Villareal ili kuimarisha kiwango chake kama alivyofanya awali kwa mfaransa Rafael Varane.

Comments
Post a Comment