Mwashiuya kukosa mechi 5 VPL


Kiungo wa timu yanga Geofrey Mwashiuya atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja na nusu baada ya kugudulika ana tatizo kwenye goti lake.

Baada ya kufnyiwa vipimo vya MRI Mwashiuya aligundulika kuwa na tatizo hilo lakini tayari ameanza kufanyiwa matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa Yanga.

Mchezaji huyo amewekewa bandeji laini ambayo inamsaidia kupona haraka ikiwa ni moja kati ya zile bandeji zinatumika katika nchi zilizoendelea.


Mwashiuya atakosa michezo mitano ya mwanzo ya ligi kuu inayotarajiwa kuanza Agosti 20 mwaka kutokana na kuuguza jeraha hilo.

Comments