Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 "Serengeti boys" itashuka dimbani leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Madagascar.
Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa taifa wa Madagascar ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika kusini.
Serengeti boys imeweka kambi katika jiji la Antananarivo, Madagascar ikijipanga vema kuikabili Afrika kusini katika mchezo wa awali kujiandaa na fainali za kombe la mataifa Afrika.
Timu hiyo itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Afrika kusini Agosti 6 mwaka na ule wa marudiano utachezwa Agosti 21 katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Comments
Post a Comment