Nolito asaini Manchester city


Baada ya kufanikisha usajili wa Kiungo wa Dortmund Ilkuy Gundogan kocha Manchester city Pep Gurdiola amekamilisha usajili wa Nolito wa Celta Vigo.

Nolito 29, ambaye pia alikuwa akiwindwa na timu ya Barcelona amesaini miaka minne kuitumikia timu ya Manchester city kwa ada ya uhamisho wa Euro 14.5 milioni.

Nolito atakabidhiwa jezi namba 9 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na mspaniola mwenzie Alvaro Negredo ambaye kwa sasa yupo Valencia.

Licha ya kuinasa saini ya Nolito bado kocha huyo Man city yupo kwenye mipango mizito ya kukamilisha usajili wa John Stone na winga Leroy Sane.

Comments