Omog ataka vifaa vipya Simba


Baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu ya Simba kocha Joseph Omog amesema anataka kusajili ili kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.

Omog amesema kuwa anataka kusajili washambuliaji wawili pamoja na mabeki wawili wa kati na tayari Simba wanakaribia kumaliza na strika wa Vital O' Laudit Mavugo.

Uongozi wa Simba umepokea ombi la kocha huyo na wamesema kuwa utamsapoti kocha huyo kwa nguvu zote ili kutengeneza Simba ya ushindani kwenye ligi.

Raisi wa Simba Evans Aveva alisema ni kweli walipokea maombi hayo na wapo kwenye mipago  ya kukaa na kocha huyo ili kufanya mazunguzo zaidi kuhusiana na usajili.

Comments