Omog ndiye kocha mpya Simba


Simba imefunga suala la mjadala wa kocha baada ya Mcameroon Joseph Omog kusaini miaka miwili kuwanoa wana msimbazi.

Kocha huyo alisaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari na raisi wa timu hiyo Evans Evans yakiwa ni masaa kadhaa kupita tangu kocha huyo atue nchini akitokea Cameroon.

Omog 44, alihaidi kuwa anazipokea changamoto zilizopo Simba na muda mfupi kuanzia sasa atayapatia ufumbuzi matatizo yote yanaoikabili  Simba.

Pia kocha huyo aliwahi kuinoa Azam kwa muda wa msimu mmoja wa mmoja na nusu hata hivyo aliondolewa na wana ramba ramba baada ya kushindwa kufikia malengo yao.

Comments