Pep kuanza mazungumzo na Bonnucci


Kocha wa Man city Pep Gurdiola anataka kumsajili beki wa Juventus Leornado Bonucci baada kuweka mpango wa kufanya nae mazungmzo wikiendi hii.

City inataka kuweka dau la Euro 43 milioni kuishawishi Juventus kumwachia nyota huyo ambaye aling'aa kwenye timu ya Italy katika michuano yaUEFA euro.

Bonucci ameonesha nia ya kujiaunga na mojawapo ya timu za ligi kuu England msimu huu na Gurdiola anaona  mchezaji huyo ni kifaa kwenye ttimu yake kama atakuwepo kwenye kikosi chake.

Bonucci 29, amekuwa muhimili katika timu ya taifa ya Italy na Juventus na timu mbalimbali England zinamwania ikiwemo Chelsea na Manchester united.

Comments