Pluijm asaini miaka 2 Yanga


Kocha wa Yanga Hans Van Der Pluijm amesaini mkataba mpya wa miaka 2 wa kuendelea kuinoa timu hiyo.

Mafanikio aliyoyapata Pluijm yanaifanya Yanga kumuongeza  mkataba mpya kocha huyo ambaye katika kipindi cha miaka miwili amepeleka neema kubwa Jangwani.

Mholanzi huyo ameiwezesha Yanga kutwaa kutwaa kombe la ligi kuu mara mbili mfululizo, kombe la shirikisho 2015/16 na kuijengea Yanga heshima kimataifa.


Comments