Pluijm kuikabidhi Yanga Ripoti ya Medeama


Kocha wa Yanga Hans van Der Pluijm leo atakabidhi muda wowote ripoti ya mchezo uliopita dhidi ya Medeama kwa uongozi wa timu hiyo.

Yanga ilifungwa magoli 3-1 dhidi ya Medeama na kudidimiza matumaini ya uelekeo wa hatua ya nusu fainali kwa timu hiyo.

Ripoti ya mwalimu Hans van Der Pluijm itahusisha matokeo ya mechi dhidi ya Medeama, ili kupata mweleko mpya wa timu katika fainali hizo za kombe la Shirikisho barani Afrika.

Hadi sasa TP Mazembe ndiye anayeongoza kundi A, akiwa na Pointi 10, ikifuatiwa na Medeama yenye pointi 5, MO Bejaia yenye pointi 5 ikiwa imezidiwa magoli ya Medeama na Yanga ikiwa mkiani kwa pointi 1.

Comments