Kocha wa mabingwa wa ligi kuu England 2015/16 Claudio Ranieri amesema kuwa nyota wa timu hiyo Riyad Mahrez anabaki Leicester city.
Mahrez 25, amekuwa akihusishwa kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na baadhi ya timu kubwa barani Ulaya kuanza kumtolea macho mchezaji huyo ikiwemo Arsenal na Barcelona.
"Nadhani kila mchezaji ambaye yuko hapa ana furaha na timu hii, kila kitu kimeisha na soko limeisha." Alisema Ranieri
Kocha huyo alipoulizwa suala la kubaki kwa Riyad Mahrez alijibu"ni kweli Mahrez anataka kubaki"
Mahrez amebakiza miaka 3 kwenye mkataba wake na huenda akaungana na Wes Morgan na Jamie Vardy ambao wamekubali kuongeza mikataba kwenye timu hiyo.

Comments
Post a Comment