Kocha wa Leicester city Claudio Ranieri amesema kuwa kocha Manchester united ndiye atakayevaa viatu kocha gwiji wa timu hiyo Sir Alex Ferguson.
Mbali na matazamo huo kocha anaamini kuwa Manchester city itafanya vizuri katika ligi ya mabingwa chini Pep Gurdiola kwa kuwa kocha ana rekodi nzuri kwenye michuano hiyo.
"Nadhani Mourinho anaweza kuwa Ferguson mpya, hawezi kudumu kwa miaka 26 lakini atafanya mambo mengi ya kocha huyo." Alisema Ranieri
Ranieri anaamini Gurdiola ni moja ya makocha waliotua sehemu sahihi ya ajira kwenye ajira yao. "Gurdiola anaonekana ni mtu sahihi mahali alipo." Aliongeza Ranieri.

Comments
Post a Comment