Sam: Sijateua nahodha mpya England


Kocha mpya wa England Sam Allardyce amesema hawezi kufanya uteuzi wa nahodha timu ya England kwa sasa hadi atakapokutana na wachezaji wote.

Sam maarufu kama 'Big Sam' alifanya mkutano na waandishi wa habari asubuhi ya leo ikiwa ni sehemu ya kuelezea na kuwasilisha mipango yake mipya kwa timu hiyo.

Hata hivyo kocha alipoulizwa kuhusu suala la uteuzi wa nahodha mpya alisema kwa sasa hana mipango hiyo hadi hapo atakapokutana na wachezaji wake wote.

"Nadhani kila kitu kitabaki kama kilivyo, siwezi kuamua nahodha wa timu kwa sasa hadi hapo nitakapokutana na wachezaji wote." Alisema Sam

Comments