Sare ya Mazembe, MO Bejaia mtihani Yanga


Huenda matumaini ya timu ya Yanga kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho yakafifia baada ya matokeo ya sare kati ya TP Mazembe na MO Bejaia.

TP Mazembe wakiwa wageni wa MO Bejaia waliweza kupata sare ya bila kufungana na waarabu hao ikiwa ni mwendelezo wa safari yao kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali.

Mpaka sasa TP Mazembe ina asilimia 90 ya kufuzu kwenye michuano hiyo ikiwa na Pointi 7, ikifutiwa na MO Bejaia yenye pointi 5, Medeama pointi 2 na Yanga ambayo ipo mkiani kwa pointi 1.

Kwa matokeo hayo Yanga inazidi kudidimia na kupoteza matumaini ya kufuzu kuendelea na fainali hizo endapo timu hizo zitaendelea kupata matokeo.

Comments