Shevshenko kocha mpya Ukraine.


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya AC Milan na Chelsea Andriy Shevshenko ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Ukraine.

Mfumania nyavu wa zamani kwa sasa ndiye atakayekuwa akiliongoza taifa lake kwenye michuano mbali mbali ya kimataifa baada ya chama cha soka nchini kufikia maamuzi ya kumteua mkongwe huyo.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'or mwaka 2004 amesaini mkataba wa miaka miwili kuiona Ukraine, pia kuna uwezekano huenda akaongezewa miaka miwili mbele kwenye mkataba.

Hii inakuwa mara kwa Shevishenko 39, kufundisha soka kwenye maisha yake tangu alipostaafu soka mwaka 2012.

Comments