Timu ya Simba intarajiwa kuingia dimbani kujipima nguvu na timu ya Burkina Faso ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Jamuhuri siku ya jumamosi.
Simba imepiga kambi yake Morogoro ikipiga mazoezi ya nguvu kujiandaa msimu mpya wa ligi na sasa kocha wa timu hiyo Joseph Omog anataka kupima nguvu kikosi chake.
Mbali na mechi hiyo Simba itacheza na Polisi Morogoro na itarudiana na Burkinafaso kwa mara ya pili ikiwa ni mechi itakayochezwa nje ya mji wa huo.

Comments
Post a Comment