Timu ya Simba itachuana na kikosi cha Inter Club ya Angola inayoongozwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Zdravko Logarusic siku ya Simba day.
Logarusic atawasili nchini siku chache zijazo akiwa na kikosi chake cha Inter Club kuwaonesha Simba ujuzi walionao.
Simba itafanya maazimisho hayo Agosti 8 kama ilivyo taratibu na desturi ya timu hiyo, safari hii ikitimiza miaka 80 tangu kuazishwa kwa timu hiyo.
Simba tayari ilikua imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya polisi Morogoro ambapo katika mchezo huo ilipata ushindi wa goli 6-0.
Logarusic alikaliliwa siku chache zilizopita kuwa na hamu ya kukutana na Simba ili kuwaonesha kwanini walimwacha kocha huyo.

Comments
Post a Comment