Timu ya Simba imetangaza rasmi kuachana na Mganda Hamis Kiiza kwenye timu yao.
Kiiza hatakuwa na simba msimu ujao baada ya kumalizana na timu hiyo ambayo imshindwa nyota huyo wa Uganda kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu.
Rais wa timu ya Simba Evans Aveva alisema kuwa wameamua kuachana na mchezaji huyo kistaarabu na wamemalizana kwa Amani.
"Tumeacha na Hamis Kiiza kwa busara na amani hivyo hatutakuwa na kiiza msimu ujao."
Kiiza ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga alifunga jumla ya magoli 19 katika ligi ya Vodacom akiwa na Simba.
Comments
Post a Comment