Sissoko aitaka ligi kuu.


Kiungo wa timu ya Newcastle Mousa Sissoko amesema kuwa anataka kurudi ligi kuu baada ya kufanya maamuzi binafsi ya kuondoka.

Sissoko 26, anatolewa macho na timu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu ikiwemo Liverpool na Arsenal ambayo ndo inaongoza kwenye ya kumwania mfaransa huyo.

"Bado nataka kubaki England, na hapa ni chaguo langu namba moja nahitaji kupata changamoto mahala pengine." Alisema Sissoko

"Si kwamba mimi ni bora sana, lakini nadhani nimefanya vitu vingi mahali nilipokuwa, na sasa nahitaji kuacha alama mahali pengine." Aliongeza Sissoko.

Newcastle ilishuka baada ya kufanya vibaya msimu ulipoita na sasa nyota huyo aliyeng'aa akiwa na ufaransa UEFA Euro anaona ni wakati sahihi wa yeye kuondoka kwenye kwenye timu hiyo.

Comments