Spurs yawaekea mzigo Intermilan

Timu ya Tottenhma hotspurs inajiandaa kuweka mzigo wa kutosha ili kufanikisha usajili wa strika wa intermilan Mauro Icardi.

Spurs inataka kuweka mezani dau la euro 38 milioni kuishawishi Intermilan kumuachia Muargentina huyo ambaye amekuwa moja ya washambuliaji bora Serie A.

Spurs inajiandaa kuweka ushindani mzito epl pamoja na kuandaa timu bora kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya na wanaona Icardi n mmoja wa wachezaji muhimu ili kuimarisha timu yao.

Icardi yupo kwenye bifu zito na mshambuliaji wa Lazio ambaye pia ni raia wa Argentina baada ya kujihusisha kimahusiano aliyekuwa mkewe na kusabisha ndoa yake kufa miaka 2 iliyopita.

Comments