Beki wa Liverpool Martin Srktel yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho kwenda Fenerbahce ya Uturuki.
Srktel 29, amekamilisha zoezi la vipimo nchini Uturuki ambapo hadi kufikia kesho dili la uhamisho wa mchezaji litakuwa limekamilika rasmi.
Liverpool imekubali dau Euro 5 milioni kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo ambaye amedumu Livepool tangu mwaka 2007 aliposajiliwa na Rafael Benitez.
Ujio wa beki Joel Matip kutoka Schackle 04 umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa mchezaji huyo ambaye Klopp alionesha dalili ya kuachana nae.

Comments
Post a Comment