Mshambuliaji wa timu ya Yanga Amis Tambwe amesema anaishukuru timu yake kwa kutambua uwezo wake alionao wa kupachika magoli.
Tambwe anasema Simba ilipoamua kumwacha Yanga walitambua uwezo wake na ndiyo maana ameionesha timu hiyo kuwa yeye ndiye mfungaji bora kwa sasa.
"Nadhani Yanga walitambua uwezo wangu, nami sitawaangusha, nimekuwa na hali ya kufunga wakati wote, nadhani simba waliponiacha wao waliona kipaji changu." Alisema Tambwe
Tambwe ameahidi bado ataendelea kupambana na kuijengea Yanga heshima huku akisisitiza kuwa matumaini yake ni kuvunja rekodi ya ufungaji Tanzania inayoshikiliwa na Mohamed Hussein 'Machinga'.

Comments
Post a Comment