Mshambuliaji wa timu ya Yanga Amis Tambwe atakua fiti kuivaa timu ya Medeama siku ya Jumamosi baada ya kupona.
Tambwe allikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria ambao ulimweka benchi wakati Yanga ikivaana na TP Mazembe ambapo katika mchezo huo timu hiyo ilipoteza mchezo huo baada ya kufungwa 1-0.
Tambwe ambaye alianza mazoezi binafsi Tangu wiki iliyopita ataungana na mwalimu Hans Pluijm kikosini baada ya afya yake kuimarika.
Uwepo wa mshambuliaji huyo katika mechi dhidi ya Medeama kesho utaongeza chachu ya ushindi kwa timu ya Yanga kutokana na kuelewana na vema na mchezaji Donald Ngoma katika safu ya ushambuliaji.

Comments
Post a Comment