TFF yamfungia Jerry Muro


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imefungia afisa haari wa timu ya Yanga Jerry Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja.

TFF imemfungia msemaji huyo kutokana na madai ya kupingana na maamuzi ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwashambulia kwenye vyombo vya habari.

Muro ambaye kwa sasa yupo kwenye mapumziko mafupi nyumbani kwao machame atatakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 3 ikiwa ni sehemu ya fedha inayombatana na kifungo hicho.

Comments