Chama cha soka nchini Ubelgiji kimemfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu hiyo Marc Wilmot baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya UEFA Euro.
Ubelgiji iliondolewa kwenye hatua ya robo fainali baada ya kufungwa magoli 3-1 na Wales licha ya kuwa Ubelgiji ilikuwa kwenye nafasi za juu kwenye viwango vya FIFA kuliko Wales.
Pamoja na kuwa na kikosi bora kilichosheheni nyota mbali mbali wanaowika Ulaya kwa sasa akiwemo Eden Hazard, Kevin De Bryune, Romeu Lukaku na Yannick Carrasco lakini bado timu hiyo ilishindwa kutamba kwenye mashindano.
Tayari chama cha soka nchini Ubelgiji kimetangaza rasmi kwamba wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayerithi kiti kilichoachwa wazi na kocha Marc Wilmot.

Comments
Post a Comment