Ureno kama zali vile UEFA Euro


Ni jambo la kushangaza lakini habari ndiyo licha ya ureno kushindwa kukosa ushindi ndani ya dakika tisini lakini wametinga nusu fainali.

Ureno ilipata sare katika michezo yote  mitatu kwenye kundi lake alipokutana na Iceland, Austria na Hungary ambapo matokeo yalimpeleka kwenye hatua ya 16 bora kwa nafasi ya best loser.

Lakini Ureno ndiyo huyo amenyanyuka baada ya kumng'oa Croatia licha ya timu kupiga mpira mwingi na jana walithibitisha kuwa nyota yao inang'aa baada ya kumng'oa Poland kwa mikwaju ya Penati kwenye hatua ya  robo fainali.

Na sasa Wareno hao wamepumzika wakimsikilizia mshindi kati ya Wales na Ubelgiji ambao wanakipiga leo, huenda maajabu yakaendelea, lakini huenda ndoto zao zikaishia hapo lakini nina imani Christiano Ronaldo anaiwaza zaidi fainali ili ajitegenezee njia nyeupe kuelekea kwenye tuzo ya dunia.

Comments