Ni mwendelezo wa nderemo na vifijo katika mitaa na vitongoji vya miji ya Ureno baada ya timu yao ya taifa kufuta makosa ya mwaka 1984,2000 na 2004 baada ya timu hiyo kutofanya vizuri katika mashindano makubwa.
Timu ya ureno imeondoka leo asbuhi nchi ufaransa baada ya kufurahia kwa kuonyesha kombe hilo walilolitwaa katka mikono ya mwenyeji ufaransa baada ya mchezaji wa akiba Eder kuacha kilio katika mitaaa ya Ufaransa.
Wachezaji wa ureno wakiongozwa na kiongozi wao, nahodha cristiano ronaldo na kocha wao santos wamepanda ndege asubuhi baada ya sherehe hiyo fupi iliyofanyika hotelini walipokuwa wanaishi timu ya ureno.
Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shwangwe kubwa.
Ureno ambayo ilicheza muda mwingi bila ya nahodha wao na mshambuliaji wa kutegemewa cristiano ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dak ya 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea kumsaidia majukumu kocha Santos katika dakika za mwisho na mwisho kulinyanyua kombe hilo.
Ronaldo amesema kombe hilo ni kwa ajili ya Wareno wote pamoja na wanaoishabikia timu hiyo.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hiyo ya taifa ya Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.
Comments
Post a Comment