Usajili Azam ni balaa


Azam imeanza kufanya fujo kwenye usajili baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa huenda kipa wa timu wa taifa wa Ivory coast akasaini kwenye timu hiyo.

Daniel Yeboah Tetchi 31, huenda akasini muda wowote kuanzia sasa kwenye timu ya Azam muda mfupi baada ya kumshusha kipa wa Tenerife ya Hispania.

Tetchi tayari yupo Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumalizana na timu ya Azam na muda wowote kuanzia sasa huenda akasaini.

Comments