Timu ya Yanga itashuka dimbani kesho kuvaana na Medeama ya Ghana katika mchezo wa marudiano na waamuzi wanatoka nchini Morocco.
Tayari tayari shirikisho la soka Afrika (CAF) ilishaingiza majina ya waamuzi wa mchezo huo mtandaoni ambapo Redouane Jiyed atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiana Mohamed Lahmidi pamoja na Hicham Ait Abbou.
Timu zote mbili hazijapata ushindi wowote katika mechi walizocheza Yanga ikiwa na Pointi 1 na Medeama ikiwa na pointi mbili hivyo kila timu inahitaji ushindi hapo kesho.
Yanga imepoteza michezo miwili dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe hivyo timu inatakiwa kufanikisha zoezi la kujipatia pointi 3 hapo kesho kurejesha matumaini.

Comments
Post a Comment