Wijnaldum amtoa macho Klopp.


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anavutika na mpango wa kumsajili kiungo wa Newcastle Gioginio Wijnaldum.

Klopp bado anataka kuongeza kwenye eneo la kiungo ambalo bado lina kasoro na anaona Mholanzi ndiyo suluhisho kujaza nafasi hiyo pale Anfield.

Mchezaji huyo wa zamani wa PSV alikuwa kwenye kiwango bora na Newcastle, licha ya kushuka daraja kwa Newcatle lakini bado baadhi ya kubwa zimeendelea kumtolea macho Wijnaldum.

Klopp anatakiwa kufanya kazi ya ziada kumng'oa Wijnaldum 25, kutokana na kocha wa sasa wa Newcastle kuweka mipango ya kuwabakiza nyota wake ili kuirudisha timu hiyo ligi kuu.

Comments