Kiungo nyota wa Newcastle Giorginio Wijnaldum anakaribia kutua Liverpool baada ya Newcastle kuridhia dau la £ 25 milioni kama ada ya uhamisho.
Wijnaldum atalazimika kusafiri kuifuata Liverpool Marekani kwa ajili ya kukamilisha zoezi la vipimo pamoja na kuungana na nyota wengine kwenye timu hiyo.
Liverpool imeondoka baada ya ushindi wa mechi ya kirafiki ilichozwa jana ambapo timu hiyo imetimka kuelekea Marekani kufanya ziara zake.
Mholanzi huyo atakua mchezaji wa sita kusjiliwa na Liverpool baada kukamilika kwa usajili wa wachezaji watano nyuma.
Comments
Post a Comment