Willian ajifunga Chelsea


Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Willian amejifunga rasmi baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka na timu hiyo.

Willian 27, ataendelea kuitumikia Chelsea hadi 2020 baada ya kukaa Chelsea kwa miaka mitatu akitokea Shakthar Donetsk mwaka 2013 kwa dau la uhamisho wa Euro 32 milioni.

Willian alisema kuwa anafuraha baada ya kusaini mkataba na timu hiyo kwa kuwa ni moja kati ya ndoto zake kuendelea kuitumikia timu hiyo.

"Nina furaha baada ya kusaini mkataba mpya na Chelsea hii ni ndoto yangu ya muda mrefu, kubaki na timu hii ni jambo linalonipa furaha."



Comments