Yanga kuifuata Medeama kesho kutwa


Timu ya Yanga inatarajia kundoka ijumaa ya kesho kutwa kuifata Medeama ya Ghana kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Kocha wa timu hiyo Hans Pluijm yupo kwenye maandalizi makali ya kikosi hicho ya kuandaa kikosi hicho kwa ajili ya ushindi dhidi ya Medeama.

Bado Yanga itaendelea kukosa huduma ya Hassan Kessy kutokana na sakata lake la usajili linaloendelea katika timu ya Simba.

Yanga yenye pointi 1 katika kundi hilo itakuwa kwenye kibarua kizito cha kukabiliana na Medeama baada ya matokeo ya nyumbani kuwa sare 1-1.

Comments