Yanga ndo basi tena.....!!

Mabingwa wa soka Tanzania bara na kombe la FA wameshindwa kutamba ugenini nchini Ghana baada ya kufungwa goli 3-1 na Mediama katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga imepoteza matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali baada ya kubakiwa na pointi moja waliyovuna katika michezo minne ambayo tayari wamecheza.

Katika mchezo huo Yanga walizidiwa katika safu ya kiungo na hivyo kuruhusu kufungwa goli tatu katika kipindi cha kwanza.
Goli la Yanga limepatikana kwa njia ya penati kupitia kwa mchezaji wao Simon Msuva dakika ya 25  baada ya mshambuliaji Obren Chirwa kudodonshwa katika eneo la hatari.
Huku mdgoli ya wenyeji wao yakifungwa na Amoah dakika ya 7 ya mchezo na Mohammed aliyefunga goli mbili katika dakika ya 23 na 37 za mchezo huo.

Comments