Wanachama na mashabiki wa Yanga wamemchangia Ofisa habari wa timu ya Simba Haji Manara kiasi cha pesa ili afanikishe mpango wake wa kutibiwa India.
Manara bado anasumbuliwa na jicho moja ambalo limepoteza ufanisi mzuri wa kuona na hivyo ameamua kuchukua uamuzi wa kwenda kutibiwa India.
Ofisa habari wa timu ya Yanga Jerry Muro amesema kuna kiasi cha zaidi ya shilingi 1,000,000 ambachi kimechangwa na mashabiki hao kwa ajili ya kufanikisha safari ya Manara.

Comments
Post a Comment