Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero huenda akafungiwa mechi tatu na kuikosa mechi ya Manchester united baada ya kumpiga kipepsi beki wa West Ham Winston Ried.
Aguero alifanya tukio hilo kwenye dakika ya 72 na kumtoa nje beki huyo ambaye alishindwa kuendelea na mechi hiyo kutokana na maumivu makali kifuani.
baadhi ya wachambuzi wamesema kuwa Mchezaji huenda akapatwa na adhabu ya kufungiwa mechi 3 ikiwemo na faini ya pesa kwa muargentina huyo,
Kwa upande wa kocha wa timu ya Manchester city Pep alisema kuwa haoni sababu ya mchezaji ya kufungiwa kwa mchezaji kwa kuwa ni tukio la bahati mbaya kwenye mchezo.
"Nadhani ni tukio la bahati mbaya kwenye mchezo, sidhani kama mchezaji atafungiwa na kukosa mechi." Alisema Gurdiola.

Comments
Post a Comment