Timu ya Manchester city imeanza vizuri katika mechi ya kufuzu kwenye hatua ya makundi champions ligi baada ya kuichapa Steaua Bucuresti mabao 5-0.
Aguero aliondoka na mpira baada ya kufunga mabao 3 peke yake huku mawili mengine yakiwekwa nyavuni na David Silva pamoja na Nolito.
City imeanza vizuri ikiwa ugenini na hiyo ni dalili njema ya wao kufuzu kuelekea kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Comments
Post a Comment