Aguero: Pep ananibadilisha, nazidi kuwa bora


Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero 'Kun' amesema ana mabadiliko makubwa tangu kocha wa sasa Pep Gurdiola alipotua kwenye timu hiyo.

Aguero amefunga jumla ya magoli 6 katika mechi tatu akizocheza, mabao 3 amefunga EPL na yale yaliyobaki alifunga dhidi ya Steaua Bucuresti katika mchuano kufuzu ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

"Nazidi kuwa bora na imara, Pep ana mbinu nyingi uwanjani, ingawa soka lake ni la kumiliki zaidi mpira hii inanipa nafasi nyingi za kufunga magoli." Alisema Aguero.

"Kuna baadhi ya mambo niliku siyafahamu, na mengine nahitaji kuyafanyia kazi, nitajituma ili niwe bora zaidi." Aliongeza Aguero.

Mbali na Sergio Aguero wachezaji wengi wa timu hiyo wamesifia ubora na ubunifu wa Pep akiwemo Gael Clichy na Fabian Delph.

Comments