Algeria kuichezesha Taifa stars v Super Eagles


Shirikisho la soka barani Afrika (caf) limemteua mwamuzi Mehdi Abid kuchezesha mechi ya kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika nchin Gabon kati ya Nigeria na Tanzania.

Mechi hiyo itachezwa Septemba 3 mwaka huu ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa uliochezwa Tanzania kuwa na matokeo ya sare.

Abid atasaidiwa na Abdelhak Etchiali ambaye ni mwamuzi msaidizi namba moja pamoja na Ahmed Tamen kuelekea uwanja wa Adokiye Amesiamaka, Port Harcout Nigeria.

Hadi sasa Misri ndiyo inayoongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Nigeria pamoja na Tanzania ambapo kwenye kundi timu ya Chad ilijitoa kwenye mashindano.

Comments