Ama kweli Julio haishiwi maneno sikia hii


Kocha wa Mwadui Jamuhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa ulikuwa sababu kubwa uliowafanya wao kupoteza mechi dhidi ya Toto Afrikaa.

Akizungumza baada ya mchezo huo julio amesisitiza kuwa goli walilofungwa halina lawama isipokuwa kuna mapungufu makubwa uwanjani.

"Uwanja wa CCM kirumba ni mbovu nadhani hauna hadhi ya kutumiwa kwenye za ligi kuu, tulifungwa goli sahihi ila mapungufu ya uwanja yamepelekea sisi kupoteza mechi." Alisema Julio

Bao pekee la Toto Afrika lilifungwa na Waziri Junior na kuyafanya matokeo kuwa 1-0 hadi mwisho wa mchezo.

Comments