Appiah: Ghana itafika nusu fainali Russia


Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amesema kuwa ana imani kikosi chake kitatinga nusu fainali kwenye fainali za kombe la dunia 2018.

Appiah ambaye alikuwepo kwenye benchi la ufundi la timu ya Ghana mwaka 2010 kwenye fainali Afrika Kusini aliongeza kuwa ana imani na vijana kwa kuwa sasa wameandaliwa kiushindani zaidi.

"Nadhani soka la sasa linahitaji nguvu na ujuzi wa hali ya juu jambo ambalo lipo kwenye bara letu la Afrika."

"Nina imani tukifuzu fainali  hizo kuelekea Russia 2018, hakuna shaka Ghana itamalizia mkia tulioshindwa kumega pale Afrika Kusini nadhani tutatinga nusu fainali." Alisema kocha huyo

Comments