Arsenal na Chelsea zimeng'arisha mbaya EPL baada ya timu hizo kuibuka na ushindi wa mabao matatu katika mechi za leo.
Arsenal ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Watford, wafungaji wa magoli hayo akiwa Santi Carzola aliyefunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.
Kwa upande wa Chelsea ambao walikuwa nyumbani dhidi ya Burnley mabao yao yalifungwa na Eden Hazard, Willian na Victor Moses.
Matokeo hayo yanaipeleka Chelsea Kileleni baada ya kukusanya pointi 9 katika mechi 3 huku Arsenal ikisogea kwa pointi nne.

Comments
Post a Comment