Timu ya Atletico Madrid jana katika uwanja wa nyumbani imeshindwa kutamba mbele ya Alaves baada kupata sare ya bao 1-1.
Atletico ilipata wakati mgumu kutokana safu imara ya ulinzi iliundwa na Alaves, licha ya Kevin Gameiro kufunga kwa mkwaju wa Penati kunako dakika ya 90, lakini Manu Garcia alichomoa bao katika muda huo wa dakika za nyongeza.
Mshambuliaji wa Atletico Kevin Gameiro kwa upande wake alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu huku akiongeza walifanya makosa kupoteza nafasi walizopata.
"Mechi ilikuwa ngumu, ilikuwa si kazi rahisi uwanjani, hata hivyo tulifanya makosa kupotez nafasi tulizopata." Alisema Gameiro.

Comments
Post a Comment