Kutokana na mipango mikubwa inayofanyika katika timu ya Simba raisi wa timu hiyo Evans Aveva amediriki kusema Simba haitakuwa na mpinzani msimu ujao.
Aveva alizungumza hayo baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Millenium Tower, eneo la makumbusho Dar es Salaam.
Simba imeanza kufufua matumaini yake baada ya bilionea Mohamed Dewji kuweka nia yake ya dhati kuwekeza kiasi kisichopungua shilingi bilioni 20 ili kumiliki asilimia 51 ya hisa kwenye timu hiyo.
Simba bado inajifua na mwalimu Joseph Omog katika mkoa wa Morogoro na wameweza kufanya vizuri katika mechi kadhaa za kirafiki.
"Tuna benchi zuri la ufundi tunaamini tutafanya vizuri pia, mwalimu Omog ameendelea kuonesha juu zake za kuandaa Simba ya ubingwa katika msimu mpya wa ligi." Alisema Aveva

Comments
Post a Comment