Mshambuliaji wa Ghana Adrew Ayew ameiga rasmi Swansea city baada ya kusaini miaka minne West Ham kwa dau la £20.5 milioni.
Ayew ambaye amedumu kwa mwaka mmoja Swansea, alisajiliwa na timu ya Wales akitokea Mersaille ya Ufaransa.
Ayew ni mmoja kati ya washambuliaji walioizoea ligi ya Uingereza na ameonesha uwezo mkubwa wa kufumania nyavu licha ya kuwepo kwa upinzani mkali EPL.
Ayew ambaye ni mtoto wa mwanasoka maarufu wa zamani Abeid Pelle alithibitisha kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa kwa sasa ni mchezaji halali wa West Ham.
Kupitia ukarasa wake wa twitter mchezaji huyo ameushukuru uongozi mzima wa Swansea pamoja na benchi la ufundi kwa ushirikiano na kuwa naye pamoja katika kipindi chote ambacho alikuwa nao pamoja.

Comments
Post a Comment