Azam chupu chupu Chamanzi jana, yatoa sare


Timu ya Azam jana ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani imeshindwa kuondoka na pointi 3 baada ya kutoa sare ya bao 1-1 na African Lyon.

Lyon ilipata bao dakika ya 46 kupitia Mayanja Abdul aliyefunga kwa mpira wa kona ambao ulipitiliza moja kwa moja wavuni.

Azam ilishambulia kwa kasi baada ya bao hilo walilofunga Lyon lakini hata hivyo Lyon walikuwa imara kulinda lango.

Hata hivyo nahodha wa Azam John Bocco alisawiza bao hilo kwenye dakika ya 90 zikiwa zimesalia sekunde chache mpira kumalizika na kuyafanya matokeo kuwa 1-1.

Comments